UIMBAJI


UIMBAJI WA VIWANGO
Jrc media Group-2015

   Kuimba ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki, tuni) au ghani-MELODY. (Singing is the act of producing musical sounds with the voice) Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba au bila vyombo vya muziki (be sung as acapella) au kwa kutumia vyombo. Mwimbaji huyo kwa lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa pia katika vikundi vya uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead singer) na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers)

    
VILAJI NA VINYWAJI
      Vilaji na vinjywaji visivyofaa Kabla ya kuimba Kuhusu chakula, ni muhimu ili kuepuka kuimba  tumbo likuwatupu kabisa. Kuimba ni kama riadha, inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia kuepuka kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na shibe.

     Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo. Kumbuka kuimba ni kazi ngumu, unahitaji mafuta (you need fuel), hivyo inashauriwa kuwa na mlo wa kawaida wa saa moja au mbili kabla ya uimbaji ni bora zaidi. Kulingana na mazoea yetu vipo vyakula na vinywaji ambavyo ni vigumu kuachana navyo ghafla, mengine huchukua muda. Lakini hata hivyo kwa ajili ya kutunza koo (Mashine inayozalisha sauti) pamoja na kujihepusha na madhara yanayoweza kujitokeza unapokuwa na shughuli nzito ya uimbaji, ni muhimu ujihepushe navyo. Nitakuambia kwa ufupi kuhusu vyakula visivyofaa unapokuwa na shughuli za uimbaji. Kwasababu za msingi si rahisi kukutajia kwa undani madhara ya baadhi ya vyakula au vinywaji, wasiliana na mwalimu kwa wakati wako. Baadhi ya vyakula na vinywaji vya kuepuka kabla ya kuimba ni kama vile:
     …… Vinavyoleta mwasho au kukera koo (throat irritants): vyakula au vinywaji vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy foods) ,  kama vile kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari iliyosafishwa, chocolate. Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya ·        

       Vyakula vinavyoongeza mucous (sehemu ya kiwambo cha seli inayozunguka mfereji wa chakula): maziwa, koni, mayai/maziwa yenye ubarafu (ice cream), maziwa mgando na aina nyingine ya maziwa (dairy products) Vyakula vinavyofanya koo kuwa kavu: matunda jamii ya machungwa, pombe Soda na aina ya vinywaji vinavyochemsha au vinavyojaza gesi au hewa katika tumbo Vyenye ubaridi sana au barafu: husababisha koo kubana, kuminywa au kunyongwa. ·        

       Vyakula, vinywaji vyenye ubarafu na pombe (ikiwa ni pamoja na mvinyo na bia). Kuna baadhi ya watu pia huwa na alegi (kwa mfano, baadhi ya waimbaji wana shida na matunda jamii ya machungwa, ngano, karanga, samakigamba au soya). ·         Vyakula vyenye mafuta mengi Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji wako zingatia : ·         Punguza  matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda ·         Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga ·         Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji ·         Punguza kuendesha gari, ongeza kutembea kwa miguu ·         Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati ·         Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika Zingatia : ·         Maji ya moto au aina ya chai mitishamba (herbal tea) ni bora,
      Mwimbaji mzuri hutumia glass 8 za maji kwa siku, wapo ambao hutumia hadi lita 4 pia yapo maji ya ziada kutoka katika vyakula. ·         Kupaaza sauti kwa kukohoa kohoa sio njia ya kukusaidia kuimba vizuri, badala yake hukata sauti ·        
     Pamoja na umuhimu wa maji, lakini acha matumizi ya maji mengi saa moja au mbili kabla ya kuanza uimbaji badala yake asali ni bora zaidi. Lakini pia sauti ikipatwa na tatizo unaruhusiwa kupata maji ya moto pamoja na asali ·        
      Angalizo kuhusu mazoezi: Mazoezi huwa yana ugumu wake hasa pale   unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili nafasi ya ku-adopt mabadiliko koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na: Aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai fulani ya mitishamba au mchaichai, kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari n.k



Pata masomo haya zaidi kupitia account ya facebook https://web.facebook.com/jifunze.muziki.5





 UMUHIMU WA CHORDS KATIKA MUZIKI
    Kwanza ni lazima tufahamu kuwa chord katika muziki ni kama mifupa katika mwili wa binadamu. Ina maana nyama bila mifupa zitadondoka tu. Hivyo na chords ni mifupa inayobeba nyama yaani sauti zote iwe za waimbaji au vyombo vya muziki. Chords ni framework. Ni frame ambapo picha huwekwa. Hivyo chords ni muhimu sana katika muziki.
    Kuna aina nyingi za chords ila tuta angalia aina ya chords 2 muhimu zidi. Mfano;
                (1) Chord kuu/ Major chords
                (2) Chord ndogo/ Minor chords

MAJOR CHORDS-KORD KUU
 CHORD KUU   ni chord iliyokamilika iliyo na noti ya msingi yaani do, na noti ya tatu mi, na notiya tano  so. 
Tutaanza mfano kutoka katika ufunguo wa C-Major yaani C-Kubwa maana ndio ufunguo rahisi zaidi kufundishia. Kwanza lazima tujue kanuni ya kupata ufunguo mkuu.
Kanuni ni;[ I+III+V ]  Yaani ni sawa na kusema noti ya I jumlisha na ya II na ya tano.
    Je! Hizi noti unazipataje? Sikiliza! Sauti za kimuziki zimepangiliwa katika mfumo wa alfabeti 7 za mwanzo yaani A, B, C, D, E, F, na G. na herufi hizi ndio hutumika katika majina ya funguo za muziki 7.
Hivyo ninaposema ufunguo wa C ni kutokana na hizo herufi. Sasa ikiwa ufunguo tuliopewa ni C-Major basi noti ya kwanza kulingana na kanuni yetu itakuwa ni C. OK?. kWA HIYO kama C ni ya kwanza sasa tunatafuta ya tatu yake na tano yake kulingana na mlolongo wa kialifabeti. Sasa itakuwa ya tatu kutoka C ni E na ya tano kutoka C ni G. Kulingana na kanuni itakuwa hivi;
                                 {I + III + V }= C + E + G
                                  C+ E  + G   =C-Major chord.    
 Na katika majina ya kitaalamu ya kimuziki yaani do, re, mi, fa, so, la, ti chord hii itatamkwa do, mi, so, ambapo     do=noti ya 1,  mi=noti ya 2,  so=noti ya 5.
Kwa watungaji nyimbo hili ndilo somo la kukomaa nalo maana ukijua misingi ya chords utaweza kutunga nyimbo yoyote na kwa mpangilio mzuri na nyimbo hazitafanana. Mimi mwenyewe mpaka sasa nimeshatunga na kufundisha nyimbo 352(miatatu hamsini na mbili) tangu mwaka 1998 na zote hazifanani kutokana na kulielewa somo la chords vizuri. Nimefundisha kwaya nyingi sana zingine nimeshazisahau. Mpaka sasa nimetunga nyimbo 57 ambazo bado sijazifundisha popote.
    
     Vilevile kwa waimbaji somo la chords ni muhimu pia kwa sababu mwimbaji akijua anaimba chord gani ataimba kwa ubora zaidi kuliko asiyejua maana hatafanya makosa kabisa kaitka uimbaji wake.

    Je kwa wapigaji vyombo vya muziki inakuwaje? Lo!! sasa mpiga vyombo mfano gitaa, kinanda,tarumbeta, violin n.k asipojua somo la chords kwa kweli ana wakati mgumu kuliko hata mfungwa wa segerea. Kabisa sisemi uongo. Mpigaji asiyejua chords ni kama dereva aliyefungwa macho maana atakosea sana.

Hapa ni jedwali linaloonyesha chords kuu na noti zake.



Asante Mungu akubariki mwanafunzi wangu. Kwa leo naishia hapa. Tuonane tena katika kipindi kijacho ambapo tutajifunza kuhusu kord ndogo
Amen. Ubarikiwe na Bwana Yesu.
                                                                
              .........................................................................................................................................

SOMO KUHUSU MFULULIZO WA KORD(CHORD PROGRESSION)
Chord ni nini? Chord ni sauti mbili au zaidi zinazosikika kwa pamoja.
Triad ni utatu yaani ni chord yenye sauti tatu tu, zinazo sikika kwa pamoja. Chord  hii ndio husababisha kuwepo kwa muafaka katika uimbaji wa sauti tatu yaani ya  kwanza nay a pili nay a tatu.
Melody ni tune. Ni sauti moja inayosikika ikiwa na mfululizo wa noti katika viwango vya sauti mbalimbali.(Pitch)
Pitch ni kiwango cha sauti kuwa juu au chini kulingana na mitetemo ya sauti.
Noti ni sauti moja kwa kipindi Fulani cha wakati.
Mfululizo wa kord(chords) ni mfuatano wa chords kwa mpangilio maalumu. Hapa chini ni mifano ya mfululizo ya chords mbalimbali.
      Mfululizo ya chords
I-IV-V-I=chord ya kwanza kwenda ya nne, kwenda ya tano, kasha ya kwanza tena
I-V-IV-I
I-V-I-IV-I
I-IV-I-V-I
Kanuni kuu ni( I+IV+V ).  Yaani chord ya kwanza, ya nne na ya tano.
Lakini kumbika kuwa chord huundwa kwa aina tatu za noti yaani
I+III+V=Noti ya kwanza, ya tatu na ya tano yaani do+mi+so=chord
Mfano chord ya C-major noti ni C+E+G=C-MAJOR CHORD.
Lakini mfululizo ikiwa ni ufunguo wa C-major hivyo itakuwa-
C+F+G     yaani kord ya I, ya IV na ya V. Hiini kanuni, lakini mifululizo hubadilika kutikana na aina ya wimbo.

Kitaalamu majina ya noti za kimuziki huitwa kama ifuatavyo.
I-    Tonic
II-   Supertonic
III-  Mediant                                                      
IV-  Submediant
V-   Dominant
VI-  Subdominant
VII- Leading note
VIII-Octave
Kwa hiyo ni vilevile hata katika mifululizo ya chords majina huwa ni hayohayo katika chords zote.
Katika somo lijalo tutajifunza mifano hai ya mfuluizo wa kord mbalimbali katika nyimbo mbalimbali.

Asante

        HISTORIA YA UIMBAJI NA MUZIKI


      Uimbaji asili yake ni mbinguni (Eze 28:13-15). Tutakapofika
      mbinguni tutaendelea kumwimbia Bwana (Ufu 15:2-4; Ufu 5:9-10).
      Hapa duniani nyimbo na muziki vilianza zamani sana baada ya
      kuumbwa kwa Adamu na Hawa “…na jina la nduguye  aliitwa Yubali;
      huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi.”(Mwa 4:1-21).

     UMUHIMU WA KWAYA KATIKA KANISA
      Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja(na kupiga vyombo vya
      muziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma
      ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za
      kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo  mpya. Kanisa ni mwili wa
      Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki
      (Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet
      4:10-11).
      Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo
      watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32).
      Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya
      huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Mtu mwenye udhaifu
      anaweza kusikia nguvu na uzima kwa nyimbo. Daudi alipopiga muziki
      roho mbaya ilimwacha Sauli (1 Sam 16:23).  Tunasoma pia kwamba
      siku moja Sauli aliingiwa na ghadhabu, chuki na kumwonea Daudi
      wivu baada ya kusikiliza maneno ya nyimbo (1 Sam 18:6-9).
      Nyimbo tunazosikiliza (redioni, katika kanda,  nk) kama hazina
      maneno yenye maadili mazuri, mioyo yetu inaweza kuchafuliwa na
      kutufanya twende kinyume na mapenzi ya Mungu.
      Nyimbo zinavuta nguvu na uwepo wa Mungu (2 Nya 20:21-22; 2 Fal
      3:15-16). Paulo na Sila waliomba na kuimba nyimbo za kumsifu
      Mungu, hatimaye milango ya gereza ikafunguka (Mdo 16:25-26).

      AINA ZA NYIMBO
      Nyimbo nyingi zinaangukia katika makundi yafuatayo
1.   Nyimbo za mafundisho/maonyo (Kol 3:16).
2.   Nyimbo za faraja

 3.  Nyimbo za mahubiri (Isa 48:20).

 4. Nyimbo za sifa/shukurani/maombi

 5. Zipo pia nyimbo za upuzi (Amo 6:5). Mungu hapendi nyimbo za upuzi.

      Biblia inatuagiza kuimba “kwa akili”  yaani tuimbe huku tukiwa na
      ufahamu wa nyimbo tunazoimba (Zab 47:6-7; 1 Kor 14:15). Kwa sababu
      hiyo, wanakwaya wanapaswa pia kujua nyimbo wanazoimba zina maana
      gani au lengo lake ni nini. Zinahubiri au zinafariji? Zinajenga au
      zinabomoa? Vinginevyo wanaweza kujikuta wanaimba nyimbo za upuzi
      au zisizokuwa na maana.

      Kama wewe mwenyewe huelewi yale unayoimba, unafikiri wale
      wanaosikiliza wimbo wako wataelewa? Sio rahisi.

      MADA ZA NYIMBO
      Wimbo unaweza kuwa na mada (topic) moja au zaidi. Lakini wimbo
      wenye mada moja ni mzuri zaidi. Kwanini?

 1.  Wimbo wenye mada moja mara nyingi unaanza kwa utangulizi,
      baadaye unaelezea mada yenyewe na kisha unatoa hitimisho,
      kwahiyo ni rahisi kukumbuka ujumbe wa wimbo huo.

 2. Unakuwa na ufafanuzi wa kutosha. Beti 3 au 4 zinazungumzia
     mada moja tu kwa kuifafanua. Mada ya wimbo inaweza kumlenga mtu mmoja au watu kadhaa:

  * Waliobatizwa

  * Mvulana na msichana waliotangazwa kwamba ni wachumba

  *Maharusi – waliofunga ndoa (Zab 78:63) nk.

  *Watu ambao hawajaokoka (wanaosikiliza mkutano wa Injili).
  “KUMECHISHA”
 Neno hilo linatumika kuelezea jinsi mtu alivyovaa mavazi
 yanayofanana rangi. Mtu anaweza kumwambia rafiki yake: “Aisee, leo
 umependeza! Umemechisha vizuri sana – kuanzia kichwani hadi miguuni!”
      Wakati wa ibada, kwaya inaweza pia “kumechisha” nyimbo zake na
      mahubiri au tukio la siku hiyo. Kwa mfano, kama mada ya mahubiri
      ni “Faida za wokovu”, kwaya itafute wimbo unaozungumzia wokovu na
      kuuimba kabla au baada ya mahubiri. Wakati wa mkutano wa Injili,
      ili “kumechisha,” pambio kama hii inafaa kuimbwa” ”Akina baba
      njoni, akina mama, njoni, nanyi vijana njoni, mje muokolewe…”
      Wimbo kama huu ufuatao haufai kuimbwa na kwaya wakati mwinjilisti
      anapokuwa amemaliza kuhubiri mkutano wa Injili: ”Sio kila mtu
      asemaye ameokoka, ataingia mbinguni. Siku ile watasema, ‘tulikuwa
      wahubiri’, watakataliwa.
      Siku moja mahali fulani kwaya ilikaribishwa iimbe wimbo ili
      kukamilisha mahubiri  ya siku hiyo. Mahubiri yalikuwa mazuri sana
      lakini bahati mbaya kwaya ile iliimba wimbo “usiomechi” na
      mahubiri yale: ”.. toa kwanza boriti katika jicho lako mwenyewe
      ndipo utoe kibanzi katika jicho la ndugu yako.” Tuimbe kwa akili
      na pia  “tumechishe”!
      Ili kwaya iweze kila mara kufaulu kumechisha inahitaji kuwa na
      nyimbo nyingi, zenye mada mbalimbali. Ni vizuri kila somo katika
      Biblia liwe na wimbo wake. Yaani ziwepo nyimbo zinazozungumzia
      wokovu, utakatifu, amri za Mungu, neema, msamaha, ubatizo, ndoa,
      watoto, utumishi, uinjilisti, maombi nk, nk. Je, kwaya ya Kanisa
      lako ina nyimbo ngapi? Sulemani alikuwa na nyimbo zaidi ya 1000 (1
      Fal 4:29-32).
      JINSI YA KUPATA WIMBO/MADA MPYA
      Watu wengi wanapenda vitu vipya. Kiatu kipya, gauni jipya, nyumba
      mpya, vyombo vipya nk. Vivyo hivyo watu wanapenda kusikia nyimbo
      mpya. Lakini je, ni rahisi kwaya au watunzi wa nyimbo kupata
      nyimbo mpya kila mara?
      Mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kupata nyimbo au mada mpya.
 1  Ukisikia sauti ya wimbo (melody) moyoni mwako fanya haraka
     kuirekodi kwenye kanda (kama una radio cassette na microphone)
     ili usisahau.
 2. Soma Biblia, soma vitabu vya Neno la Mungu. Hudhuria vipindi
     vya mafundisho. Mada unazozipata zitungie nyimbo. Nyimbo
     zinazotungwa kwa njia hii ni nzuri kwa sababu zinalingana na
     Neno la Mungu.  Sio rahisi watu kuzikosoa kwamba haziendani na Biblia.

 3   Unaposafiri, unapokuwa sokoni nk, sikiliza yale yanayosemwa,
      tazama yanayofanyika kisha uyatungie nyimbo (za maonyo, za
      ushauri nk) kulingana na Neno la Mungu.

 4.Mwombe Mungu akupe wimbo mpya. Mungu anaweza yote.
    Unapokosa maneno ya kuweka katika wimbo sio vizuri kujaziajazia tu
    maneno au sauti zisizo na maana ili wimbo uimbike!
     UPIGAJI WA VYOMBO VYA MUZIKI
      Maneno ya nyimbo yanavutia sana yanapoambatana na upigaji mzuri wa
      vyombo. Biblia inatuagiza tupige kwa ustadi (Zab 33:3). Kila
      inapowezekana tuwe tayari kujiunga na shule za muziki au kujifunza
      kwa wale wanaojua ili tuweze kupiga vyombo kwa ustadi. Siku hizi
      kwenye mtandao kuna masomo mengi ya muziki yanayotolewa bure
      kuhusu jinsi ya kupiga gitaa, kinanda, jinsi ya kusoma noti za
      muziki(notation) nk. Tuwe tayari kuyatafuta.
      Biblia inasema tusiifuatishe namna ya dunia hii (Rum 12:2a). Hata
      katika uimbaji na upigaji wa vyombo hatuna haja ya kuifuatisha
      namna ya dunia hii. Haimpi Mungu utukufu ukisikia mtu anasema:
      “Kwaya hii imeimba wimbo unaofanana na wimbo wa yule msanii wa
      muziki kule Marekani (ambaye hajaokoka).” Tunaye Mungu anayeweza
      kutusaidia kupiga vyombo kwa ustadi. Tumtegemee.
      Vyombo vya muziki vinasaidia kubeba ujumbe. Kwahiyo fundi mitambo
      wa Kwaya ni vizuri ahakikishe kwamba sauti za vyombo hazizidi zile
      za waimbaji. Vinginevyo watu watasikia tu vyombo na kukosa ujumbe.
      MITINDO YA UIMBAJI
      Kuna mitindo mbalimbali ya uimbaji. Wengine wanaimba huku
      wamesimama wima, wengine wanaimba huku wamekaa, na wengine
      wanaimba huku wakionesha ishara mbalimbali kwa mikono na miguu
      yao. Mitindo ya uimbaji ni mizuri iwapo tu inasaidia kufikisha
      ujumbe kwa wahusika. Huduma ya uimbaji sio “show.” Hatuimbi ili
      kuwaonesha wengine kwamba sisi tuna mitindo mizuri ya kuimba.
      Kwahiyo kwa mfano, kama wimbo una maneno yafuatayo: ”Dunia
      inaangamia. Watu hawamchi Mungu, asubuhi mpaka usiku watu
      wanakunywa pombe, wanafanya uzinzi, wanapigana. Tuwaombee
      wasiangamie…” sio vizuri kuuimba wimbo huo kwa mitindo ya shangwe
      na nyuso zilizojaa furaha. Sio vizuri kwa sababu sio jambo
      linalofurahisha kuona watu wanaangamia.

       UTAKATIFU KATIKA UIMBAJI
      Huduma ya uimbaji ni muhimu iendane na maisha ya utakatifu. Mizaha
      wakati wa mazoezi ya nyimbo haifai. Mizaha ni dhambi (Mit 26:19,
      19:29; Zab 1:1).
      Kuimba bila utakatifu ni kelele mbele za Bwana (Amo 5:12, 22-23).

      Wanakwaya ni walimu. Wanalifundisha Kanisa. ”Basi wewe
      umfundishaye mwingine, je! hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye
      kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? Wewe usemaye kwamba mtu
      asizini, wazini mwenyewe?…” (Rum 2:21-24).

      UMUHIMU WA KUIOMBEA KWAYA
      Ni muhimu kuiombea kwaya bila kukoma. Pasipo Mungu Kwaya haiwezi
      kufanya hayo tuliyojifunza katika somo hili (Yn 15:5). Kwahiyo
      basi tuwaombee viongozi wa kwaya, walimu wa kwaya, wapigaji wa
      vyombo nk. Tukemee roho ya kiburi na mafarakano isipate nafasi
      katika kwaya. Tuwaombee watunzi wa nyimbo, Bwana awape nyimbo mpya
      zenye ujumbe mzuri. Tuviombee vyombo vya kwaya visiharibike.
      Tuwaombee wanakwaya wawe na bidii ya kumtumikia Mungu kwa uimbaji
      (Rum 12:11).
       MASOMO HAYA PIA YANAPATIKANA KATIKA https://web.facebook.com/jifunze.muziki.5

19 comments:

  1. Ubarikiwe sana mwalimu! Nimejifunza kitu hapa.

    ReplyDelete
  2. Mimi naendelea kukufatilia kwa makini karibu sana

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli nami nimebarikiwa sana Mwalimu,shida yangu kubwa nataka kujua kusoma Nota,yaan hili ndilo hitaji langu kubwa Kwa sasa,maana natunga nyimbo tena nzuri na zenye maudhui,Ila Nota sijui,msaada wako tafadhali,namba yangu 0686-424260 ipo Hadi WhatsApp, ubarikiwe

    ReplyDelete
  4. Hichi kitabu kinapatikana wapi

    ReplyDelete
  5. Asante sana teacher , namna gani naweza pata PDF

    ReplyDelete
  6. Asante sana naweza kupata Kwa mfumo wa pdf

    ReplyDelete
  7. Amina mtumishi,nimebarikiwa sana,

    ReplyDelete
  8. MUNGU akubariki sana 🙏🏼

    ReplyDelete
  9. Ubarikiwe sana MTU wa MUNGU, Umenijenga sana kabisa.

    ReplyDelete
  10. Franckstyvefranck@gmail.com

    ReplyDelete