Asante Juliana Biblia inatuagiza kuimba "kwa Roho" na “kwa akili” yaani tuimbe huku tukiwa na ufahamu wa nyimbo tunazoimba (Zab 47:6-7; 1 Kor 14:15). Kwa sababu
hiyo, wanakwaya wanapaswa pia kujua nyimbo wanazoimba zina maana
gani au lengo lake ni nini. Zinahubiri au zinafariji? Zinajenga au
zinabomoa? Vinginevyo wanaweza kujikuta wanaimba nyimbo za upuzi
au zisizokuwa na maana.
Kama wewe mwenyewe huelewi yale unayoimba, unafikiri wale
wanaosikiliza wimbo wako wataelewa? Sio rahisi. Hivyo ni lazima kujifunza kuimba kwa ustadi sana Roho mtakatifu hapendi sauti mbaya au muziki mbaya maana yeye ndiye muasisi wa muziki ulio bora
No comments:
Post a Comment