Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja (na kupiga vyombovya muziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma ya
uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za kuvutia na uwezo wa
kutunga nyimbo mpya. Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi; na kila
kiungo kina kazi. Kiungo hiki (Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa
litahudumiwa (1 Pet 4:10-11). Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la
Kale walikuwepo watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya
6:31-32).
No comments:
Post a Comment