ETI MCHUNGAJI NINI UMUHIMU WA KWAYA KANISANI?
Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja(na kupiga vyombo vyamuziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma
ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za
kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo mpya. Kanisa ni mwili wa
Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki
(Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet
4:10-11). Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo
watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32).
Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya
huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Mtu mwenye udhaifu
anaweza kusikia nguvu na uzima kwa nyimbo. Daudi alipopiga muziki
roho mbaya ilimwacha Sauli (1 Sam 16:23).

Ameen Asante sanaa nimepata kitu
ReplyDeleteMmmh. Mbona hatuoni mitume wakiwa na kikundi Chao Cha kwaya. Haya makwaya yameigwa kutoka ulimwengu kama vikundi vya kusherehesha tuh
ReplyDelete