Monday, 30 January 2023

Monday, 5 December 2022

Friday, 10 April 2020

MAJOR PENTANTONIC PRINCIPLE


MAJOR PENTANTONIC PRINCIPLE


BABA MIMI NAITWA ELIAS SEGESELA NIKO LUHOTA IRINGA NAOMBA KUJUA KANUNI YA PENTATONIC SCALE
Asante Elias kamwene. Kanuni ya msingi ni kuwa katika ngazi kuu ya pentatonic/Pentatonic major scale ni kwamba hakuna noti ya IV yaani (fa) na noti ya VII yaani (ti) hivyo inakuwa
Do, re, mi, so, la, na kuna noti tano tu ndiyo maana inaitwa pentatonic yaani neno "penta" ina maaana "tano"

Thursday, 9 April 2020

DIFFERENCE BETWEEN CUBASE PRO 9 AND LOGIC PRO 9


DIFFERENCE BETWEEN CUBASE PRO 9 AND LOGIC PRO 9

MWALIMU MIMI NAITWA ABEY MUSSA NATOKA SUMBAWANGA RUKWA SASA NATAMANI SANA KUJUA KUTUMIA PROGRAM YA LOGIC PRO 9 JE HAINA TOFAUTI SANA NA CUBASE PRO 9?
Hakuna tofauti kubwa sana katika operation hasa katika mpangilio ispokuwa Logic pro 9 inahitaji super computer kwa ajili ya speed zaidi maana ina vitu vingi sana

MEANING OF DYNAMICS IN MUSIC



MEANING OF DYNAMICS IN MUSIC

MTUMISHI UBARIKIWE SANA KWA MASOMO MAZURI MIMI NAITWA CAROLINE SAMMY NIKO IGUGUNO SINGIDA NAOMBA KUJUA MAANA YA DYNAMICS KATIKA MUZIKI
Amen sana Caro Dynamics katika music ni mabadiliko ya sauti yaani volume aidha kuwa kubwa au ndogo kulingana na mahitaji ya muziki au kipande cha muziki hapa chini nimeweka mifano baadhi ya kuonyesha maneno yanayotumika kuonyesha mabadiliko ya sauti katila muziki

LINES AND SPACES ON STAVES


LINES AND SPACES ON STAVES



MKUU MIE NAITWA GUSTAV NATOKA NEWALA NAOMBA KUJUA NJIA RAHIS YA KUKARIRI MAJINA YA MISTARI YA STAFF
Katika stave ya treble au bass mistari na nafasi zake hukaririwa kwa maneno au sentensi ambapo kila herufi huwakilisha jina la mstari au nafasi katika stave nimekuwekea mifano hai hapo juu

PROPER RIGHT HAND ON BASS GUITAR



PROPER RIGHT HAND ON BASS GUITAR
MTUMISHI NAITWA MOSES NIKO ARUSHA NISAIDIE UPIGAJI MZURI WA BASS GITA KWA RIGHT HAND
Hapa chini namekuwekea picha kuonyesha jinsi ya upigaji sahihi wa bass gita

NOTES AND RESTS


NOTES AND RESTS

TICHA NAITWA FERDY TOKA DODOMA NAOMBA KUJUA AINA ZA MAPUMZIKO YA NOTA KATKA MUZIKI
Sawa Fredy hapa chini nimekuwekea aina za nota na mapumziko yake "Rests"

Friday, 20 March 2020

CHORD SUBSTITUTION


CHORD SUBSTITUTION


MIMI NAITWA GEOPHREY NATOKA MKOA WA SIMIYU SWALI LANGU NI KUJUA KIKAMILIFU KUHUSU "CHORD SUBSTITUTION"
OK! Chord substitution ni mfumo wa kutumia chord nyingine badala ya chord husika katika mfululizo wa chord ambapo chord hiyo ina uhusiano na chord halisi ili kupata ladha nzuri zaidi katika muafaka wa mfululizo wa chord kwa mfano mfululizo wa ii V7 IM7 mfano katika Bb, ii ni Cm, V ni F7, na I ni Bb kwa hiyo tritone ya F ni B hivyo B7 ni substitute badala ya F7 kwa hiyo ina -resolve katika Bb M7 au Bb6 na kanuni hii huitwa Dominant substitution kwa maana hutumia noti ya Vb kupata substitute chord ambayo huwa mbadala wa chord ya V katika mfululizo huo na chord hii ya substitution hutmika kama passing chord kwenda IM7 au I6 au I9 kwa jina lingine huitwa chromatic passing chords. Asante Geophrey!

Wednesday, 11 March 2020

E7#9#5 CHORD



https://youtu.be/HzcrjjwdPjo

MIMI NIKO KIGOMA NAITWA STEPHANO MWALIMU NAOMBA UNIPE KANUNI YA CHORD YA E7#9#5 NA INAVYOTUMIKA
Sawa mshiko wa E7#9#5 ni hivi hapo chini na hutumika kama altered passing chord kwenda Am9 nusu tone juu na nusu tone chini ni Em7b5(b13)

Tuesday, 10 March 2020

MASTERING WITH WAVES PLUGINS


MASTERING WITH WAVES PLUGIN
 
https://youtu.be/b1-zJaODztc

JINA LANGU NI SEBASTIAN NIKO SINZA MIMI NI PRODUCER NISAIDIE MKUU EQ GANI NI NZULI KWA VOCAL MASTERING
OK! Sikiliza EQ zote ni nzuri ila inategemeana sana na seetting yako ya vocal room na mic uwezo wa mic yako na hata sikio lako liwe zuri pia lakini mimi hutumia waves plugins na EQ ninayotumia ni kwa vocal mastering ni API lakini situmii preset zake nafanya setting kulingana na production yangu. Karibu sana Sebastian

Saturday, 7 March 2020

KUIMBA KWA ROHO NA AKILI



https://www.youtube.com/watch?v=QKG2C0AZrFY

MIMI NAITWA JULIANA NIKO MOROGORO ETI PASTOR KUIMBA KWAYA INATOSHA TU ROHONI AU LAZIMA KUWA NA UJUZI ZAIDI
Asante Juliana Biblia inatuagiza kuimba "kwa Roho" na “kwa akili” yaani tuimbe huku tukiwa na ufahamu wa nyimbo tunazoimba (Zab 47:6-7; 1 Kor 14:15). Kwa sababu
hiyo, wanakwaya wanapaswa pia kujua nyimbo wanazoimba zina maana
gani au lengo lake ni nini. Zinahubiri au zinafariji? Zinajenga au
zinabomoa? Vinginevyo wanaweza kujikuta wanaimba nyimbo za upuzi
au zisizokuwa na maana.
Kama wewe mwenyewe huelewi yale unayoimba, unafikiri wale
wanaosikiliza wimbo wako wataelewa? Sio rahisi. Hivyo ni lazima kujifunza kuimba kwa ustadi sana Roho mtakatifu hapendi sauti mbaya au muziki mbaya maana yeye ndiye muasisi wa muziki ulio bora

Friday, 6 March 2020



https://youtu.be/bb6XS_5sUq4

MWALIMU MIMI NAITWA DANIEL NAOMBA UNIELEZE INTERVALS NI NINI?
Interval ni umbali au nafasi iliopo kati ya noti moja kwenda nyingine mfano interval kati ya C na D ni 2nd interval au intavali ya II n.k

Thursday, 5 March 2020

ALTERED PASSING CHORDS



https://youtu.be/HzcrjjwdPjo

https://youtu.be/PzPhIOKdcpk

MIMI NAITWA MUSTAPHA NIKO MBEZI KIMARA NAOMBA KUJUA NINI MAANA YA ALTERED PASSING CHORD NA INATUMIKAJE
Asante Mustapha Altered passing chord hutumika tofauti na dim7 ambayo hutumika nusu tone kwenda juu mfano Db dim7
ni passing chord kwenda Dm7 lakini Altered passing chord yenyewe huwa nusu tone zaidi ya chord husika na kanuni yake ni kupandisha nusu tone/ku-sharp note ya tano na ya tisa ambapo hiutwa #9#5 mfano C7 noti ya tisa ni D na ya tano ni G kwa hiyo itakuwa C+E+G#+Bb+D# hii ni C#9#5 Altered

Wednesday, 4 March 2020

CADENCES AND USE


https://youtu.be/HzcrjjwdPjo
MIMI NAITWA FANUEL NATOKA MOSHI WILAYA YA ROMBO SWALI LANGU KUNA AINA NGAPI ZA CADENCE NA MATUMIZI YAKE
Kuna aina nne za cadence katika music composition nazo ni kama ifuatavyo; 1. Cadence kamilifu/perfect cadence hutumika ktk mfululizo wa V-I. 2. Cadence danganyifu/Deceptive cadence hutumika ktk mfululizo wa V kwenda chord yoyote isipokuwa I. Mfano V-VI . 3 Cadence ya Amen/Plagal cadence hutumika ktk mfululizo wa IV-I . 4. Cadence isiyo kamilifu/Imperfect cadence hutumika ktk mfululizo wa chord yoyote kwenda V. Asante Fanuel

Saturday, 29 February 2020

COMMON SEVENTH JAZZ CHORDS


https://youtu.be/PzPhIOKdcpk

MTUMISHI MIMI NAITWA MARCUS NATOKA MUSOMA NAOMBA UNIJULISHE CHORD ZA JAZZ NI ZIPI?
Safi sana kord zinazotumika sana katika muziki wa jazz ni zile zilizoongezwa note ya saba yaani seventh kwa hiyo chord zote mfano Major seventh, Minor seventh, Dominant seventh, Diminished seventh, na Half Diminished seventh n.k hizi zote hutumika sana katika muziki wa jazz

Wednesday, 26 February 2020

UMUHIMU WA KWAYA KANISANI



https://youtu.be/PzPhIOKdcpk
ETI MCHUNGAJI NINI UMUHIMU WA KWAYA KANISANI?
Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja(na kupiga vyombo vyamuziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma
ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za
kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo mpya. Kanisa ni mwili wa
Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki
(Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet
4:10-11). Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo
watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32).
Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya
huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Mtu mwenye udhaifu
anaweza kusikia nguvu na uzima kwa nyimbo. Daudi alipopiga muziki
roho mbaya ilimwacha Sauli (1 Sam 16:23).

Saturday, 22 February 2020

DOMINANT SUBSTITUTIONS


https://www.youtube.com/watch?v=QKG2C0AZrFY
MWALIMU NAOMBA KUJUA "DOMINANT SUBSTITUTES RESOLUTION NA KANUNI ZAKE" Dominant substitutes hu-resolve nusu tone chini yake na hutokana na chord ambayo ilkuwa substitute note ya tano au "Tritone" Mfano Tritone ya G ni Db hivyo Db7 ni subtitute ya G hivyo inaresolve katika C6 ambayo ni Tonic kwa hiyo Domint substitute chord inatumika kama passing chord mfano tena (Eb7 resolve to Dm7, Ab7 resolve to G7 n.k n.k)

Wednesday, 19 February 2020

THE USE OF BLUES SCALE


https://youtu.be/b1-zJaODztc
NAOMBA MSAADA WAKO TICHA JUU YA MATUMIZI YA BLUES SCALE
Blues scale hutumika katika upigaji wa chord za minor ambazo huwa na msingi wa chord kuu zenye mfumo wa Dominant seven mfano (17, IV7 na V7)

Tuesday, 18 February 2020

SOLO GUITAR PROFESSIONAL



https://www.youtube.com/watch?v=3l3RMne6c2o
NITACHUKUA MDA GANI?Ili uweze kupiga solo lazima uanzie kupiga rhythim kwanza ili vidole vyako viweze kulainika zaidi ndipo uanze kujifunza misingi ya upigaji wa solo gitaa itahitaji muda wa kutosha kumudu gitaa hilo

VOCAL RECORDING CUBASE 5

https://www.youtube.com/watch?v=3l3RMne6c2o

https://www.youtube.com/watch?v=QKG2C0AZrFY
MKUU NATAKA KURECORD VOCAL NIMEWEKA MIC 3 NATUMIA CUBASE 5 LAKINI VOCAL ZINAKUJA KWA NJIA MOJA NIFANYAJE?
Sikiliza ndugu! Ingia kwenye "Devices" kisha "VST Connections" au bonyeza 'F4" kisha Add Bus stereo utaona itakuja Bus name chagua mono 2 na mono 3 utakuwa umeruhusu njia ya mic zako ikiwa unarecord mono track

ANIMATION ADOBE PHOTO CSS3



https://www.youtube.com/watch?v=3l3RMne6c2o
MCHUNGAJI NAOMBA KUULIZA ETI NAWEZA NIKAFANYA ANIMATION KUTUMIA ADOBE PHOTO CS3?
Nikweli unaweza kufanya animation nenda>>window>>Animation>>kisha chagua>>convert to time line au frame animation ila kwa ushauri wangu ni vyema ukatumia Adobe after effect kwa matokeo mazuri zaidi



DIAPHRAGMATIC BREATHING




https://www.youtube.com/watch?v=QKG2C0AZrFY
https://www.youtube.com/watch?v=3l3RMne6c2o
MWALIMU. MIMI NI MWMBAJI NATAMANI NIWEZE KUIMBA VIZURI JE NIFANYEJE MWALIMU?
Ili uweze kuimba kwa ubora mkubwa ni lazima mapafu yako yaweze kutunza punzi nyingi na pia uweze kutumia misuli ya tumbo wakati wa kuimba au (Diaphragmatic singing) Punzi inahitaji mazoezi maalumu ya upumuaji wa kutumia Diaphragm yaani (Diaphragmatic breathing) pia ujue ni vyakula gani na vinywaji gani vinafaa kwa mwimbaji wa viwango haya yote ukija Jrc Elite School ndiyo jibu lako

Friday, 23 August 2019

KWAYA NI NINI?


https://www.youtube.com/watch?v=3l3RMne6c2o

Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja (na kupiga vyombovya muziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo mpya. Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki (Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet 4:10-11). Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32).

Thursday, 22 August 2019

NI MAMBO GANI NIZINGATIE ILI NIWE PRODUCER MZURI?


https://www.youtube.com/watch?v=3l3RMne6c2o

2. Jitahidi kuwa mtu mwaminifu na kuwajali watu kila wakati
3. Uwe na ujuzi wa kuwajenga wasanii waweze kukuamini
4. Uwe mbunifu katika kutunga mistari na kuimba ili wasanii wakuamini zaidi
5. Jenga mazingira ya kujali kazi ya msanii iwe nzuri na siyo kupata pesa tu
6. Uwe tayari kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana bila kujali kupoteza usingizi wako
7. Wakati mwingine uwe tayari kujitolea kumbeba msanii endapo umegundua kuwa anakipaji
8. Uwe mtu wa malengo usiridhike na kiwango ulicho nacho tamani kufika mbali zaidi
9. Jitahidi uweze kujua kucheza ala za muziki mfano gitaa, kinanda, trumpet n.k maana itakupa ujuzi zaidi wa kuboresha kazi zako
10. Tafuta ladha yako ushangaze ulimwengu acha kuigiliza ladha za wengine kuwa na "touch" yako ikutambulishe kimataifa.
CIAO

Tuesday, 30 July 2019

COMMON PASSING CHORD




NI AINA GANI YA PASSING CHORD AMBAYO NI COMMON SANA?
Aina ya passing chord ambayo ni common sana ni Diminished 7 hii huleta ladha nzuri sana mfano unapotoka chord ya C kwenda A-minor kanuni inaruhusu kutumia Ab Diminished 7 kwa kuwa Ab ni half step lower than A-minor jaribu uone ladha yake ni kiungo kizuri sana

Friday, 19 July 2019

AUDIO MUSIC COMPRESSION



JE NI LAZIMA NITUMIE AUDIO COMPRESSOR KWA KILA INSTRUMENT?
Hapana si lazima ufanye compression kwa kila kitu na ni muhimu ujue nini maana ya compressor na matumizi yake yaani wakati gani utumie compressor au usitumie na ni vizuri kujua ni aina gani ya compressor unapaswa kutumia.ila katika final mix yako yaani master ni vizuri kujifunza kutumia serial compression katika audio chain yako

PARALLEL MOTION IN NOTATION



PARALLEL MOTION NI NINI KATIKA MUZIKI?
Parallel motion ni aina ya mwenendo wa noti za muziki katika mwelekeo mmoja ziko aina nyingi za mienendo ya noti katika muziki na hapo chini ni mfano wa parallel, contrary, na oblique motion

Tuesday, 2 July 2019

VYAKULA VYA MWIMBAJI




JE! ILI NIWE MWIMBAJI WA VIWANGO NINAHITAJI VYAKULA VYA AINA GANI?
Mwimbaji wa viwango anahitaji kuwa makini sana katika matumizi ya vyakula maana kuna vyakula vingine na hata vinywaji ambavyo ni hatari kwa afya ya mwimbaji. JRC MEDIA tunajitahidi sana kufundisha kuhusu afya ya sauti ya mwimba yaani (Vocal Health Care) Fuatilia somo hili katika blog yetu kuhusu waimbaji http://jrcmedia.blogspot.com/p/blog-page_6.html

Monday, 1 July 2019

AUTO TUNE INATUMIKAJE

AUTOTUNE KAZI YAKE NI NINI?
Hii inatumika katika vocal kubadilisha tone ya sauti ya mwimbaji inakuwa laini na ya kuvutia lakini husaidia kubalance pitch ya sauti iliyo nje ya key ubaya wake kama mtu hajui kuimba anaimba flat itaharibu sana vocal kwa wasiojua kuimba inawasadia pia

VARIAUDIO JINSI YA KUTUMIA

VARIAUDIO NI NINI KATIKA CUBASE 5?
VariAudio ni mfumo katika programme ya cubase kukuwezesha ku-tune sauti iliyo nje ya pitch ikae katika pitch inavyotakiwa na mfumo huu umesaidia sana kwa wale ambao hawawezi kuimba katika pitch wanaohamahama key lakini hii ni nzuri tu pale mtu anahama pitch kwa kiasi kidogo

Sunday, 5 May 2019

ANACRUSIS


ANACRUSIS NI NINI?
Ni pigo au mapigo ya noti yasiyo ya mkazo ambayo hutangulia kabla ya kipimo/bar ya kwanza ya pigo la mkazo. Mfano hapo juu.

Thursday, 2 May 2019

PIANO CHORDS


Chord ni nini? Ni mlio wa sauti mbili au zaidi zinazosikika kwa pamoja. Ziko chord za aina nyingi na hutumika kwa matumizi yenye mpangilio maalum mfano chord inayoitwa Diminished yenyewe hu-resolve katika tonic na mara nyingi hutumiwa pia kama passing chord

Friday, 26 April 2019

KAZI YA WAVE COMPRESSOR





KAZI YA WAVE COMPRESSOR NI NINI?
Kazi yake ni kushusha signal zinazidi na kupandisha signal za audio zilizo chini kwa kutumia setting zake mfano threshold au ratio au attack au release au gain n.k

Wednesday, 24 April 2019

OCTAVE


Octave ni mjumuisho wa sauti nane yaani kutoka Do  mpaka do' ya juu. Oct maana yake ni nane kwa hiyo Octave ni sauti nane

Tuesday, 23 April 2019

TEMPO TRACK KATIKA CUBASE 5



JE! UNAWEZA KUBADILISHA TEMPO YA WIMBO KATIKA CUBASE 5?
Ndiyo unaweza kufanya hivyo kwa kutumia Tempo track na ukabadilisha tempo yoyote unayotaka.

Wednesday, 17 April 2019

MIDI CONTROLLER KEYBOARD


MIDI Controller ni kinanda kinachotumia mfumo wa mawasiliano ya elektronic na software za muziki katika computer ili kutengeneza muziki

Friday, 12 April 2019

PASSING CHORDS



Ni chord isiyo husika na mfululizo wa chord za familia moja yaani Non diatonic chords hutumika kuunganisha chord mbili za familia moja yaani Diatonic chords

CIRCLE OF FIFTH / GURUDUMU LA UTANO




Ni mfumo rahisi wa kukariri chords kwa kuruka chord tano tano mfano C hadi G ni chord tano hii ni katika major na minor chords

Saturday, 6 April 2019

MAANA YA MASTERING



Matering ni kitendo cha kuweka effects mfano compressor katika master bus/ sterio out bus pia kubalansi sauti katika level inayotakiwa kwa commercial